Taarifa tunazokusanya
Tunaweza kuhifadhi taarifa za akaunti, duka, matawi, watumiaji, bidhaa, mauzo, matumizi, madeni, ripoti, taarifa za kifaa na activity logs zinazohitajika kuendesha mfumo.
Matumizi ya taarifa
Taarifa hutumika kutoa huduma za DukaPoint, kuandaa ripoti, kudhibiti ruhusa, kutuma notifications zilizoidhinishwa, kutoa support na kuboresha usalama wa mfumo.
Utenganishaji wa taarifa
Taarifa za biashara hutenganishwa kwa utambulisho wa duka na tawi. Watumiaji hupata taarifa kulingana na akaunti, nafasi na ruhusa walizopewa.
Analytics na cookies
Kurasa za umma za DukaPoint hutumia Google Analytics kupima idadi ya wageni, kurasa zinazotembelewa na vitendo kama kubonyeza WhatsApp, kupakua app au kutuma form ya maombi. Google Analytics inaweza kutumia cookies na taarifa za kifaa au eneo la jumla. Takwimu hizi hutumika kuboresha website na huduma; hatutumii Analytics kuonyesha taarifa za siri za biashara ndani ya dashboard.
Huduma za nje
DukaPoint inaweza kutumia huduma za nje kama Google Analytics, SMS provider, hosting na YouTube kwa video za mafunzo. Huduma hizo zinaweza kupokea taarifa zinazohitajika kutekeleza huduma husika, kwa mfano taarifa za matumizi ya website, namba ya simu na ujumbe wa SMS.
Usalama na muda wa kuhifadhi
Tunatumia udhibiti wa akaunti, ruhusa na kumbukumbu za shughuli kupunguza matumizi yasiyoidhinishwa. Taarifa huhifadhiwa kwa muda unaohitajika kutoa huduma, kutimiza wajibu wa biashara na kushughulikia migogoro.
Haki na mawasiliano
Kwa swali, marekebisho au ombi kuhusu taarifa zako, wasiliana na AkiliTech Africa Limited kupitia derick5877@gmail.com au +255 717 364834.
Ilisasishwa: 17 Oktoba 2026
Rudi DukaPoint