DukaPoint Logo DukaPoint

Mfumo wa usimamizi wa duka, supermarket na bar kwa biashara ya kisasa

DukaPoint ni mfumo unaosaidia wamiliki wa biashara kudhibiti stock, mauzo, mikopo, matumizi, pesa za bank, reports za siku na mwezi, pamoja na uendeshaji wa bar kwa counter, tokens, reconciliation na faida.

Umejengwa kwa ajili ya biashara zinazohitaji uwazi, uhalisia wa takwimu na control kamili ya shughuli za kila siku.

Trial ya siku 7 inapatikana kwa wateja wapya

Kwa biashara gani?

  • Maduka ya kawaida
  • Supermarkets, hardwares, stores, maduka ya vyombo, maduka ya nguo, pembejeo na vifaa vya umeme
  • Bar, pub na lounge
  • Biashara zote zinazonunua na kuuza bidhaa
  • Biashara zinazotaka reports sahihi kila siku

Kwanini uchague DukaPoint?

Tumelenga mambo ambayo wamiliki wengi wa biashara huyaumiza kila siku: upotevu wa stock, kutokujua faida halisi, reports zisizoeleweka na ukosefu wa uwazi kwenye mauzo.

Rahisi kutumia

Muonekano wa mfumo umejengwa ili mmiliki, manager au counter aweze kuuelewa kwa haraka bila mafunzo marefu.

Reports sahihi

Ripoti za siku, mwezi, bidhaa, matumizi, bank, mikopo na faida zinakupa picha halisi ya biashara yako.

SMS Alerts

Pata taarifa za bidhaa zinazokaribia kuisha na report za siku zinapofungwa moja kwa moja kwa SMS.

Inafaa biashara nyingi

Unaweza kutumia mfumo huu kwenye biashara yeyote inayonunua na kuuza bidhaa.

Huduma kuu za mfumo

Mfumo huu unaleta usimamizi wa karibu wa biashara kuanzia stock hadi report za mwisho wa siku.

Usimamizi wa Stock

Sajili bidhaa, fuatilia stock iliyopo, ongezeko, matumizi ya bidhaa na historia ya mabadiliko ya stock kwa usahihi.

Mauzo na Mikopo

Rekodi mauzo ya kawaida, ya mkopo, malipo ya madeni na aina tofauti za malipo kwa muonekano unaoeleweka.

Reports za Biashara

Pata ripoti za siku, mwezi, bidhaa, mauzo, matumizi, faida, bank na taarifa nyingine muhimu kwa maamuzi ya biashara.

SMS Notifications

Mfumo hutuma SMS kila bidhaa inapokaribia kuisha, na pia hutuma SMS ya ripoti ya siku kila report inapofungwa.

Packages za bei

Chagua package inayolingana na ukubwa wa biashara yako. Bei hizi ni za mwezi na zimepangwa ili kila aina ya biashara iweze kuanza kwa urahisi. Trial ya siku 7 inapatikana kwa wateja wapya wanaotaka kuanza kwa majaribio.

Duka Dogo

Tsh 10,000
kwa mwezi
  • Inafaa kwa maduka madogo yanayoanza
  • Stock, mauzo, matumizi na reports
  • SMS alerts za muhimu

Duka Kubwa

Tsh 45,000
kwa mwezi
  • Inafaa kwa supermarket, store au biashara kubwa
  • Ufuatiliaji wa shughuli nyingi kwa ufanisi
  • Best choice kwa operations zenye volume kubwa

Jinsi mfumo unavyofanya kazi

Mtumiaji anaanza kutumia mfumo kwa hatua rahisi na zinazoendana na utaratibu halisi wa biashara ya kila siku.

1

Sajili biashara

Fungua mfumo na sajili duka, supermarket au bar yako pamoja na watumiaji muhimu wa biashara.

2

Ingiza stock

Sajili bidhaa au vinywaji na weka stock ya mwanzo ili mfumo uanze kufuatilia mzunguko wa bidhaa zako.

3

Fanya mauzo

Rekodi mauzo ya kila siku, mikopo, malipo, matumizi na shughuli nyingine kulingana na aina ya biashara yako.

4

Pata reports

Fuatilia faida, stock, pesa za bank, matumizi na ripoti za siku au mwezi kwa maamuzi sahihi ya biashara.

Features kwa kila aina ya biashara

DukaPoint haipo kwa biashara moja tu. Kila kundi lina features zinazoendana na utendaji wake wa kawaida.

Kwa Duka

  • Kuuza bidhaa kwa urahisi
  • Kufuatilia stock na matumizi
  • Ripoti za siku na mwezi
  • Madeni na malipo ya wateja

Kwa Supermarket

  • Support ya volume kubwa ya bidhaa
  • Ufuatiliaji wa shughuli nyingi kwa pamoja
  • Reports za kina kwa management
  • Muundo unaofaa kwa operation kubwa

Kwa Bar

  • Store stock na counter stock
  • Tokens za mauzo na reconciliation
  • Breakage, returns na adjustments
  • Reports kwa counter, kinywaji na siku

Sehemu ya Bar

Kwa bar, mfumo una support owner na counter kwa mtiririko wa kazi unaofanana na uhalisia wa biashara.

Gawa vinywaji kutoka store kwenda counter tofauti tofauti.
Tumia tokens kufuatilia utoaji wa vinywaji na mauzo ya counter.
Simamia breakage, adjustments, returns na reconciliation kwa uwazi.
Pata reports za mauzo kwa counter, kwa kinywaji, kwa siku na kwa token.

Unaweza kuanza leo

Ukiwa na biashara ndogo, ya kati au kubwa, tunaweza kukuelekeza package inayokufaa na kukusaidia uanze kutumia mfumo huu kwa haraka.

Maswali ya mara kwa mara

Haya ni baadhi ya maswali ambayo wateja wengi huuliza kabla ya kuanza kutumia mfumo.

Mfumo unafaa kwa biashara gani?

Unafaa kwa maduka ya kawaida, supermarkets, stores, hardwares, pembejeo, vifaa vya umeme, Duka ya nguo,Duka la Vyombo,pamoja na bar, pub na lounge.

Bei ni ya mwezi au mwaka?

Bei zilizoonyeshwa ni za mwezi: duka dogo Tsh 10,000, duka la kati Tsh 25,000 na duka kubwa Tsh 45,000. Ada inalipwa kwa miezi 3, 6 au 12.

Mfumo unatuma SMS?

Ndiyo. Mfumo unatuma SMS notifications kwa bidhaa zinazokaribia kuisha na pia ripoti ya siku kila report inapofungwa.

Naweza kutumia kupitia simu?

Ndiyo, mfumo unaweza kutumika kupitia simu, tablet au computer kulingana na mazingira ya biashara yako.

Kwa upande wa bar kuna nini maalum?

Kuna owner menu na counter menu, stock ya store na counter, tokens za mauzo, reconciliation, reports na control ya breakage.

Nianze vipi?

Wasiliana nasi kwa maelezo ya package, setup ya mfumo, au tumia button za mawasiliano zilizopo kwenye page hii.